Ndugu wateja wa Dudumizi, kama tulivyowataarifu kwenye salamu ya ujumbe wa mwaka mpya juu ya kuwepo kwa kusudio la kuhama kwa ofisi za Dudumizi. Tunayo furaha kukutaarifu kuwa, ofisi za Dudumizi zimehama kutoka kwenye eneo la zamani ambapo ilikuwa Gates of Paradise Hotel kuja kwenye ofisi mpya kabisa hapa Shamo Park House, lakini bado tupo hapahapa Mbezi Beach.

 Ndugu wateja, lengo kubwa la kuhama kwa ofisi toka Gates of paradise kuja hapa Shamo Park House ni kutuwezesha kuboresha huduma zetu. Lengo kubwa la Dudumizi ni kuwa kampuni inayoaminika kwenye kutoa huduma bora kabisa za IT hapa Tanzania. Hivyo, kwenye utoaji wa huduma hii, inabidi kuongeza muingiliano na wateja wetu na eneo la ofisi linachukua nafasi kubwa, na hii ni moja ya sababu ya kuhama kwetu.

 

Nje ya ofisi mpya za Dudumizi.

 Shamo Park House, siyo tu, inatoa nafasi kwa wateja kufika kiurahisi, pia ina huduma zote muhimu zinazohitajikwa ili kuwapatia wateja wetu huduma bora zaidi kama ulinzi uliobora, eneo kubwa la kupaki magari , pia mazingira mazuri kwa wafanyakazi.

 Hivyo basi, tegemea mambo mengi bora kwa mwaka huu wa 2015 toka hapa Dudumizi.

 

Anuani mpya:

Kwa Gari: Kama unatoka mjini, unapofika kituo cha mabasi cha Goig, upande wako wa kulia utaona jengo la Shamo Park House, ila ili kufika, utatakiwa kwenda mita kama mia mbili na kupiga U Turn au uingie service Road na kuja kwenye jengo.

 

  Kituo cha basi Goig.

Kwa wanaokuja kwa usafiri wa jumuia (Public Bus / Daladala)

Ukiwa unatoka mwenge, basi shuka kituo cha basi kinachoitwa Goig, hapo utaangalia mbele yako na kuona jengo la Shamo Park house.

 

Ni mategemeo yetu, ujumbe huu utapokelewa kwa furaha zaidi na wateja wetu wote. Twende kazi sasa.

 

Mkata Nyoni

Managng Director

Dudumizi Technologies LTD

Search your Domain

 

Follow us on Facebook

  • Website Hosting

  • 80000Tsh

  • /Year
    • 1Gb Web Space
    • Unlimited Email Accounts
    • Free Website Builder
  • Subscribe
Call us now