Dudumizi is a leading Website Design, Hosting & Mobile Development Company in Tanzania.  As our July 2018 resolution, Dudumizi is going to change business strategy and put more focus on our current and future Innovative products, you can see full list of our products here https://dudumizi.com/products.html 

 

FEMALE: Product marketing manager 

Description:

We are looking for a Product Marketing Manager to lead our outbound marketing activities. You’ll be responsible for presenting our products in ways that will strengthen our brand and boost sales.

For this role, you be a creative and quantitative thinker. You should be familiar with various product marketing techniques, like email campaigns, dealing with vendors, pricing strategies and more.

Your goal will be to develop and implement the most profitable plans to position and promote our products to clients and other service providers.

If you love working with digital technology and are interested in using your marketing and IT skills in a creative way, this could be the ideal job for you. Using your confidence and creativity you will market Dudumizi products across channels like websites, apps and through social media. You will also be responsible for maintaining Company social media pages.

Position Type: Full Time

Location: Dar Es Salaam , Kinondoni, Tegeta Nyuki

Application Deadline: 7-06-2018


Responsibilities:

 • Prospect for potential new clients and turn this into increased business.
 •  Research and build relationships with new clients.
 • Set up meetings between client decision makers and company’s practice leaders/Principals.
 • Plan approaches and pitches.
 • Study company products
 • Translate technical details into benefits for the user
 • Follow and analyze market trends to position products
 • Develop product marketing strategies (pricing, advertising, product launching)
 • Craft compelling messages across marketing channels (landing pages, ad campaigns)
 • Work with various teams (design, content, acquisition, product, sales) to implement strategies
 • Test marketing product features, releases and ad copy
 • Evaluate projects using relevant KPIs and feedback from existing and prospective customers

Skills, interests and qualities

 • Proven experience as a Product Marketing Manager, Brand Manager or similar role
 • Background in design and copywriting is a plus
 • Experience in market analysis
 • Familiar with product marketing tactics (e.g. integrated marketing campaigns)
 • Working knowledge of web analytics tools (Google Analytics, WebTrends)
 • Excellent communication skills
 • Keen eye for detail
 • Creativity
 • Analytical mind and strong quantitative skills
 • BSc/BA in Marketing, IT, Communications or similar field

Salary

Negotiable according to your skills set. Also, you will have a Good Bonus base on performances

 

Graphic Designer

Position Type: Full Time

Location: Dar Es Salaam , Kinondoni, Tegeta Nyuki 

Application Deadline: 07-06-2018

 

Responsibilities

 • Design products artworks & images
 • Design magazine layout
 • Design Logo, brochure, catalogs and other promotions materials.
 • Work with developers to deliver a polished final products
 • Design Social Marketing banners
 • Design all company materials 

Requirements:

 • Extensive knowledge of Adobe Photoshop, Indesign and Illustrator
 • High-quality work, with attention to detail
 • Social Marketing video animation skills is added advantage 

 Salary

Negotiable according to your skills set. Also, you will have a Good Bonus base on performances

 

 If you are Interested, please send your CV and Cover letter to This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

Wanafunzi wa vyuo vikuu pamoja na sekondari, wana mchango mkubwa sana katika ukuaji wa sekta ya kenolojia ya habari. Moja ya changamoto wanayokutana nayo ni kazi zao kutoweza kuonekana au kutumika kwa uma. Hivyo, siku ya mwisho huishia kuwa historia na jamii kutonufaika na kazi hizo ambazo kama zingepata nafasi ya kutumia, zingeweza kuboreshwa na kuwa na mchango mkubwa kwa uchumi wa taifa letu.

Moja ya sababu inayowafanya wanafunzi wengi washindwe kupandisha kazi zao online ni kushindwa kumudu gharama za hosting. Katika kulitatua hili kivitendo, Dudumizi kupitia Duhosting, tunakuletea kifurushi mahususi kwa ajili ya wanafunzi (Mwanachuo Plan), kifurushi hiki rasmi kwa ajili ya kufanya hosting kwa kazi ambazo zimetengenezwa na wanafunzi wenyewe, iwe ni final year year project, iwe ni kwa ajiili ya kujifunzia.

Kwa gharama za kawaida, mwanachuo utaweza kununua kifurushi cha 1GB, email, .tz domain na Unlimited bandwith kwa 50,000Tsh tu. Habari njema ni kuwa, kifurushi hiki huweza kupatika hadi bure kabisa pindi ukitupatia ushahidi kuwa hauna uwezo wa kulipia na pia kazi yako ni nzuri na ina manufaa kwa jamii. Hivyo tuandikia kwenda This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. ukifafanua project yako unayofanya, ila hauna uwezo wa kulipia hosting, nasi baada ya kuipitia tutakuwezesha.

Moja kati ya maombi ambayo tumekuwa tukiyapokea sana kutoka kwa wateja wetu ilikuwa ni huduma ya Reseller plan. Wateja wengi walikuwa wanataka nao wajiajiri kuitia Web Hosting. Ili kuanza kutoa huuma ya Reseller plan, kunahitajika kuweka sawa mambo mengi, ikiwemo ya kimfumo na kiutendaji kazi ili kuweza kuwahudumia wateja wa moja kwa moja, na wale wanaokuja kupitia kwa resellers.

 Reseller plan ni moja ya huduma ya Website Hoting ambapo muhusika ananunua plan kwa bei nzuri na yeye kwenda kuwauzia wengine kwa gharama anazoziweka yeye. Kwa lugha ya haraka tunaweza kusema, reseller ni kama kununua kwa bei ya jumla na wewe ukaenda kuuza kwa bei ya rejareja.

Reseller plan, ni mahususi sana kwa wale wanaohitaji kuanza kufanya biashara ya Web Hosting ila hawana uwezo wa kumiliki server zao wenyewe, au hawana timu ya kutosha kuchunga server zao.

Tofauti na shared hosting, reseller hosting inakupa uwezo wa kuhost unlimited domains kwenye account moja, na wewe ukaanza kuziuza kwa wengine kwa ghara nafuu au ya juu kulingana na mfumo wako wa kibiashara.

Kwa sasa, kuna aina tatu za reseller plan ambazo tunazo, nazo ni Mama Nyoni Plan, Kinjeketile Plan na Mkwawa Plan, tumezipa majina haya ili kuwaenzi ama viongozi ama watu muhimu kwenye maisha yetu. Hii inaendana na umuhimu wa Reseller Plan.

 

Makundi ya Reseller Plan, unaweza kulipia kwa mwezi na kwa mwaka. Unapolipia kwa mwaka, gharama huwa za chini zaidi.

 

Features za kwenye reseller

 

FAQ:

Je reseller ni kwa ajili ya makampuni pekee?

Hapana, reseller ni kwa ajili ya mtu yoyote mwenye utayari wa kuanza kufanya biashara ya Website hosting

Je ninaweza kulipa Hosting ya Reseller kwa mwezi?

Niyo, kwa kifurushi cha reseller, unaweza kulipia kwa mwezi au kwa mwaka, ingawa kama utalipia kwa mwezi gharama zitakuwa pungufu  zaidi.

Je ninaweza kuhost akaunti zaidi ya moja kwenye Reseller Plan?

Ndiyo, todauti kati ya reseller na shared account ni kuwa, kwenye reseller, hakuna ukomo wa akaunti unazoweza kuhost. Ingawa tutachunga kiwango cha matumizi ya hazina za server kulingana na matumizi. Hivyo, inashauriwa usijaze akaunti nyingi kwenye plan moja.

 

Blogspot ni moja kati ya majukwaa maarufu yanayotumika kwa ajili ya kuwapa watumiaji uwezo wa kufikisha habari kupotia blog. Hapa Tanzania, blog nyingi sana zimepata umaarufu kupitia blogpost. Kuna blog kama Issa Michuzi, Mjengwa blog na nyinginezo zimekuwa chachu sana kwa wana habari na kuwafanya nao kuanzisha blog zao.

Blogspot ina faida nyingi, ikiwemo urahisi wa utumiaji, kutokuwa na gharama ya uendeshaji kwa matumizi ya kawaida, hakuna gharama ya hosting kama haujavuka ujazo, nk, ingawa pia kuna hasara zake kama kutokuwa na umiliki wa moja kwa moja na taarifa zako kitu kinachowakimbiza wengi sana, pia kuna changamoto kwenye ukuaji wake pale unapoamua kuanza kumiliki website rasmi badala ya blogspot.

Unapojiunga na mtandao wa blogspot, utaweza kutumia anuani yenye jina la kwao, mfano dudumizi.blogspot.com, matumizi haya siyo tuu yanakufanya uonekane haupo makini (kuna watakaosema ameshinwa hata kununua domain name, kweli ataweza kuaminika?), bali ni ngumu kukumbukika kwa watumiaji wako.

Mfano unamomuambia mtu jina la website au blog yangu inaitwa dudumizi.blogspot.com, kuna wengine wanaweza kuandika blogsport baala ya blogspot. Na pia, kuna wengine hawatoitembelea kwa kudhani bado haujajiandaa mpaka unatumia vya bure.

Hivyo basi, moja ya njia unazoweza kutumia kuongeza uthamani wa blog yako ni kwa kutumia domain inayojitegemea (custom domain) na ukaingunisha na blogspot, hivyo siku ya mwisho watembeleaji watatumia jina la domain yako, domain hii mfano inaweza kuwa dudumizi.com, webhosting.co.tz nk. Kwa kutumia domain kama hizi utaweza kuziunganisha na kuachana na matumizi ya jina la blogspot.

Ili uweze kufanikisha hili, hatua ya kwanza kabisa unatakiwa kununua domain name, unaweza kupata domain yako kupitia duhosting.co.tz. Baaa ya hapo, utatakiwa kusajili blogspot yako kwenye blogger.com na ukaanza kuziunganisha.

Video chini inakuongoza hatua kwa hatua jinsi gani ya kununua na kuunganisha domain yako pendwa na blogspot.

Siku hizi, utengenezaji wa website umekuwa rahisi sana, kuna programu nyingi zinazoweza kukusaidia kutengeneza website, mfano wake ni kama Joomla, WordPress, Drupal nk. Kama ilivyo sehemu nyingine, utengenezaji huu wa Website huwa na matokeo chanya endapo kutakuwa na mipango thabiti kabla ya uanzaji wa utengenezaji wake. Hii inamaanisha kuwa, unatakiwa kufahami vitu msingi kwa website kabla haujaanza kutengeneza au kutafuta mtu wa kukutengenezea.

Katika mipangilio hii, kuna vitu vitakuwa vinafanya kazi chini kwa chini (behind the scene) na kuna vile ambavyo vinaonekana/kutumiwa moja kwa moja na wateja. Muunganiko wake, ndiyo huleta matokeo chanya yatakayokupendeza. Hebu tuangalie vitu hivyo;

1. Web hosting inayoaminika na ya uhakika (Reliable Website Hosting)

Web hosting mara nyingi hufananishwa na mwenye nyumba anayekukodisha frame kwa ajili ya biashara, inakuwaje endapo kila siku nyumba yake imefungwa, inavuja au mlango wa kuingilia wateja ni kadogo hivyo kusababisha msururu wa foleni kwa wateja wanaotaka kuingia madukani.

Web hosting company ya uhakika itahakikisha website yako ipo online muda wote na hata ikitokea imeenda offline, basi ni muda mchache na haijirudii rudii, pia watakuwa wanakupa ushauri pale kunapotokea matatizo na kuhakikisha usalama wa website yako. Haijalishi umetengeneza kwa mtindo gani, hakikisha unapa hosting ya uhakika kulingana na mahitaji yako, iwe ndiyo unaanza na ukachukua kifurushi kama cha Mikumi kinachopatikana Duhosting au kwa wale wenye wateja wengi wakaamua kutumia VPS au cloud, hosting lazima iendane na mahitaji yako. Kuna makala tumeandika Ufahamu Juu Ya Website Hosting Na Tofauti Zake inaweza kukusaidia kukupa mwanga pindi unapotaka kuchagua aina ya hosting inayofaa kwa website yako.

2. Content Management System (CMS)

CMS inakusaidia kuchunga website yako kwa urahisi, CMS ipo kwenye kundi la vitu vinavyofanya kazi chini kwa chini kwa sababu ni admin hutumia kwa ajili ya kufanya maboresho kwenye website. Kwa sasa kuna CMS nyingi na hata unaweza kuamua kutengeneza ya kwako mwenyewe kama wewe ni mpenzi wa code, ila kama utaamua kutumia nyingine zinazopatikana, zipo CMS kama WordPress, Joomla nk. CMS zimesababisha utengenezaji wa website kuwa rahisi sana kwa sababu huja na template kabisa zenye muonekano mzuri.

Ingawa CMS zimeleta uchanya mkubwa kwenye anga ya website, ila pia, zimeleta changamoto kubwa ya usalama kwa watengenezaji goigoi ambao hupachika kila kitu wanachokiona, na pia kuna wengine huokota cms majalalani na kutengenezea website ambazo siku za mwisho huwa si salama na wadukuzi huzivamia na kufanya watakalo.

3. Search Engine optimization (SEO)

Kwa dunia ya sasa, kufanya SEO ni kitu cha lazima, hii ni kwa sababu ushindani umekuwa mkubwa sana, leo hii kuna mamia ya website zinazofanya kitu kimoja, na tena ujio wa Internet umeondoa mipaka, unajikuta ushindani hauishii kwenye mipaka ya Tanzania peke yake, bali unashindana na watu kutoka dunia nzima. Hivyo, ni lazima upambane.

Kumbuka, kila mtu anataka kutokea kurasa ya kwanza kwenye matokeo ya utafutaji wa Google, hivyo si kazi rahisi. Mfano mzuri, Dudumizi tumekuwa kurasa ya kwanza kwa miaka zaidi ya mitatu kwa huduma zetu za Website Design, Website Hosting na hata Domain registration hii ni kwa sababu ya kuifanyia kazi SEO.

Siku hizi, SEO imebadilika sana, unatakiwa sana kuzingatia ubora wa taarifa zako unazoweka mtandaoni, kujua keywords zako, na pia kuhakikisha website yako inafunguka hata kwa watembeleaji wa simu (Mobile ready).

4. Mobile friendly

Takwimu zinaonesha kuwa, watembeleaji zaidi ya 50% wanatumia simu za mkononi kutembelea website, hivyo ni lazima uhakikishe kuwa website yako inafunguka vyema kwenye vifaa vy amkononi kama simu, tablet, laptop ndogo nk. Ukiwa na webiste inayoonekana vyema kwenye vifaa vya mkononi pia itakusaidia sana kwenye SEO kwa kupata maksi zaidi, Google hupenda kurasa zinazosomeka vyema na vifaa vya mkononi.

5. Analytic

Huna usemi wanasema, kama hautopima, basi ni ngumu kuja kuboresha. Analytic zinakusaidia kujua muenendo wa website, pia inakupa taarifa juu ya watembeleaji wanakujaje, hutembelea page zipi na huondokea page zipi, hii inakupa nafasi hata ya kujua wapi uweke tangazo gani.

Tunapoangolea analytic, ni tofauti sana na zile zinazoonesha idadi tuu, mara nyingi wateja wetu wamekuwa wanasema nataka counter kwenye website yangu. Ukiwa na counter pekee, haitotosha kukupa taarifa nzuri zaidi. kwenye analytic unaweza kutumia Google Analytic ambayo pia inapatikana bila gharama yoyote ya ziada.


6. Kuunganisha na Mitandao ya kijamii

Siyo lazima uwepo kwenye mitandao yote ya kijamii, bali unatakiwa kuchagua ile unayoweza kuimuda na kuunganisha na website yako, makala utakuwa unazituma kutokea kwenye website kwenda kwenye mitandao jamii, mtu anayetembelea website yako awe na uwezo wa kuona nini kinaendelea kwenye mitandao jamii. Huu muuunganiko utahakikisha wateja wako wanapata taarifa zenye kujitosheleza na kukuongezea maksi zaidi.

Nini kinafuata?

Baada ya kujua vitu vya muhimu kwenye website, sasa utakuwa na shauku ya kuwa na Website yako, unaweza kupata quotation hapa, na kama utataka kuwa na hosting, tembelea Duhosting.

Search your Domain

 

Follow us on Facebook

 • Website Hosting

 • 80000Tsh

 • /Year
  • 1Gb Web Space
  • Unlimited Email Accounts
  • Free Website Builder
 • Subscribe
Call us now